Watu wawili wanahofiwa kuaga dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la abiria kugongana ana kwa ana na lori la kusafirisha mafuta katika eneo la Mundika kaunti ya Busia.
Basi hilo lilikuwa likitoka Busia kuelekea Mombasa, ajali hiyo ilipotokea katika barabara ya Busia – Kisumu.
Serikali ya kaunti ya Busia imetuma huduma za dharura katika eneo la mkasa, kufuatia ajali hiyo.
Basi hilo lilikuwa limewachukua abiria saba mjini Busia, na ilitarajiwa kuwachukua abiria wengine katika vituo mbali mbali, ikielekea Mombasa.
Wandeshaji magari wanaotumia barabara hiyo wanashauriwa kutumia barabara mbadala ili kuepuka msongamano mkubwa wa magari ambao umesababishwa na ajali hiyo mbaya.
Tutawaletea maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo kwenye taarifa zetu za baadaye.