Watu 9 wafariki katika ajali Narok

Marion Bosire
2 Min Read

Watu 9 wamethibitishwa kufariki kutokana na ajali ya gari ya kubeba abiria ya kampui ya Narok safari sacco, iliyotokea karibu na eneo la Ratili, Narok Kusini kaunti ya Narok.

Kulingana na ripoti ya polisi wa kituo cha polisi cha Mulot, ajali hiyo ilitokea saa moja usiku jana Juni 29, 2024 kwenye barabara kuu ya kutoka Bomet kuelekea Narok.

Taarifa hiyo inaelezea kwamba dereva wa gari hiyo ya uchukuzi wa abiria yenye nambari ya usajili “KDP 951K” aina ya Toyota Hiace ni mmoja wa waliofariki.

Alikuwa anasafirisha abiria kutoka Narok kuelekea Bomet na alipokaribia eneo la ajali, tairi moja ya nyuma upande wa kulia ikapasuka akashindwa kudhibiti gari.

utokana na hali hiyo gari hilo lilibingiria mara kadhaa na kusimamia kwenye mtaro.

Watu wazima wanane sita wa kiume na wawili wa kike walifariki papo hapo huku mtoto wa kike ambaye umri wake haukufahamika mara moja na wanaume wawili wakikimbizwa katika hospitali ya Longisa.

Mtoto huyo wa kike alifariki punde baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo huku wanaume hao wawili wakisalia kulazwa na majeraha makali.

Miili ya waliofariki imewekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo ya Longisa ikisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Gari hilo ambalo liliharibika pakubwa liliburutwa hadi kituo cha polisi cha Ololulunga.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *