Watu 8 wafariki kwenye ajali ya ndege Marekani

Maafisa wa kijeshi wamesema ndege hiyo ilianguka saa tano na dakika 20 saa za nchi hiyo, ilipokuwa ikifanyiwa majaribio katika uwanja wa jeshi la wanahewa la Edwards.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 8 wafariki kwenye ajali ya ndege Marekani.

Ndege moja aina ya B-52 bomber imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka kituo cha kijeshi kusini mwa Carolina na kusababisha vifo vya watu wanane.

Maafisa wa kijeshi wamesema ndege hiyo ilianguka saa tano na dakika 20 saa za nchi hiyo, ilipokuwa ikifanyiwa majaribio katika uwanja wa jeshi la wanahewa la Edwards.

Miongoni mwa wale waliokuwa kwenye ndge hiyo ni pamoja na wanakandarasi wa serikali na maafisa wa kijeshi, na wafanyakazi wawili wa kampuni ya Boeing.

Kulingana na naibu kamanda wa kitengo cha kufanya majaribio katika uwanja wa Edwards Kanali James Hayes, alisema baada ya kuangalia video ya kuanguka kwa ndege hiyo, ilibainika hakuwa ambaye angeweza kunusurika.

“Tumewapoteza raia wanane wa Marekani, ” alisema Hayes, akidokeza kuwa maafisa wanajizatiti kufahamisha familia za waathiriwa.

Haikubainika mara moja chanzo cha ajali hiyo, huku uchunguzi ukitarajiwa kuchukua muda wa hadi miezi sita.

Kwa sasa kituo hicho kimesitisha shughuli zake kwa muda.

Share This Article