Angalau watu 71 waliaga dunia katika ajali ya barabarani Jumapili iliyopita eneo la Sidama nchini Ethiopia.
Yamkini lori lilikuwa limewabeba watu kupindukia, waliokuwa wakitoka kuhudhuria harusi, wakati lilitumbukia mtoni.
Dereva wa lori hilo alipoteza mwelekeo na kuteleza kwenye daraja kisha likatumbukia mtoni.
Kamishna wa polisi katika mkoa wa Sidama amesema walioangamia ni pamoja na wanaume 68 na wanawake watatu.
Ethiopia ni miongoni mwa mataifa yanayonakili visa vingi vya ajali za barabarani barani Afrika.