Watu 5 wafariki Migori kufuatia ugonjwa wa kipindupindu

Martin Mwanje
1 Min Read

Watu watano wamefariki katika kaunti ya Migori baada ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kwa muda wa wiki mbili zilizopita. 

Akithibitisha maafa hayo, Waziri wa Afya wa kaunti hiyo Julius Awuor Nyerere alisema maafa hayo yalishuhudiwa baada ya walioambukizwa kukosa kufika hospitalini kwa wakati mwafaka.

Nyerere aliongeza kuwa ugonjwa wa kipindupindu kwa Sasa umekita kambi katika maeneo ya ufuo wa Ziwa Viktoria na maeneo ya kuchimba migodi katika kaunti ya Migori.

Alitoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari ili kulemaza kusambaa kwa ugonjwa huo.

Nyerere aliongeza kuwa kwa sasa, wanaendea kufuatilia maambukizi zaidi katika kaunti ya Migori.

Kisa cha kwanza kilichoshukiwa kuwa cha ugonjwa wa kipindupindu kiliripotiwa katika kaunti hiyo wiki mbili zilizopita.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *