Watu 47 wamejeruhiwa kwenye ajali ya iliyotokea mapema Ijumaa katika barabara ya Muhoroni eneo la Londiani kaunti ya Kericho.
Abiria hao walikuwa kwenye basi lilipopoteza mwelekeo na kuanguka .
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu 7 waliokuwa kwenye basi hilo hawakupata majeraha yoyote huku majeruhi 47, wakipelekwa katika hospitali ya Fort Tenan na magari ya kaunti ya Kericho pamoja na yale ya EMS ya shirika la Posta nchini.