Idadi ya watu walioangamia kwenye mkasa wa moto wa lori la mafuta katika barabara ya Gulu-Kampala wilayani Wakiso, Jumanne iliyopita imepanda na kufikia 24.
Kulingana na Moses Byaruhanga naibu Inspekta Mkuu wa Polisi nchini Uganda amesema waliofariki ni pamoja na wanaume 18 na wanawake 6.
Shughuli ya kutambua miili inaendelea kupitia kwa utathimini wa msimbojeni baada ya watu hao kuungua vibaya kiasi cha kutotambulika.
Watu hao walienda kuchota mafuta baada ya lori la kusafirisha mafuta kupinduka na kushika moto .
Kulingana na polisi moto huo ulisababishwa na jiko la mkaa lililokuwa limewashwa karibu na eneo la ajali.
Serikali ya Uganda imetangaza kutoa msaada wa shilingi 175,000 za Kenya sawa na shilingi milioni 5 za Uganda, kwa kila aliyefariki ili kusaidia katika mazishi.