Watu 219 wamefariki Kenya kutokana na mafuriko

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya watu 219 wameripotiwa kuaga dunia kufikia Jumamosi Mei 4 kutokana na mafuriko kote nchini Kenya.

Watu tisa walifariki siku ya Ijumaa kutokana na athari za mvua ya masika inayonyesha .

Kwa jumla watu 164 wamejeruhiwa huku wengine 72 wakikosa kujulikana waliko baada ya kusombwa na mafuriko.

Watu 206,240 wameathiriwa na mafuriko kote nchini huku familia 41,248 zikilazimika kufurushwa makwao.

Serikali imetenga kambi 115 katika kaunti 19 zinazowahifadhi jumla ya watu 27,856.

Idadi ya shule zilizoathirika na mafuriko imefikia 1,967.

TAGGED:
Share This Article