Watu 19 wauawa Gaza wakisubiri msaada

Marion Bosire
1 Min Read

Yamkini wapalestina 19 wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa na wanajeshi wa Israel katika ukanda wa Gaza, shambulizi lililolenga raia waliokuwa wakisubiri msaada kusini mashariki mwa mji wa Gaza.

Haya ni kulingana na wizara ya Afya ya Gaza na vyombo vya habari.

Gaza City, Gaza’s Ministry of Health and its Media Office said.

Taarifa rasmi ilielezea kwamba shambulizi hilo la jana Jumamosi lilitekelezwa karibu na mzunguko wa Al-Kuwait.

Ilielezea pia kwamba wanajeshi hao wa Israel walianza kufyatua risasi kuelekea kwa watu hao ambao walikuwa na njaa na ambao walikuwa wakisubiri msaada mbali na eneo ambalo wangechukuliwa kana kwamba wanahatarisha usalama.

Mahmud Basal msemaji wa idara ya ulinzi wa raia huko Gaza alisema kwamba risasi nyingi zilifyatuliwa kwa raia na kwamba majeruhi walipelekwa katika hospitali ya Ahli Arab.

Wengi wao walipokea matibabu nje ikitizamiwa kwamba mfumo wa huduma za afya Gaza unakumbwa na matatizo na unakaribia kusambaratika.

Jamaa mmoja ambaye alishuhudia shambulizi hilo aliambia wanahabari kwamba wanajeshi wa Israel walifyatua risasi kuelekea kwa umati huo na kusababisha vifo vya wengi.

Nusu ya wapalestina walio katika ukanda wa Gaza wanakumbwa na njaa hali ambayo huenda ikasambaa hadi eneo la kaskazini kufikia mwezi Mei iwapo hatua hazitachukuliwa.

Share This Article