Jumla ya watu 169 wamefariki kutokana na mafuriko kote nchini kulingana na ripoti iliyotolewa na wizara ya usalama wa kutaifa.
Kwa mjibu wa ripoti hiyo kaunti zilizoathirika zaidi kwa mafuriko ni Nairobi, Tana River, West Pokot na Homa Bay.
Kaunti za Muranga na Nakuru zimeathirika na mafuriko huku watu 66 wakiaga dunia kutokana na visa kadhaa vya maporomoko ya ardhi katika kaunti hizo.
Takriban watu 190,942 wameathiriwa na mafuriko nchini huku familia 30,099 zikiachwa bila makao .