Watu 13, wamethibitishwa kufariki na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani, iliyotokea katika eneo la Cheptangule, kaunti ya Bomet.
Ajali hiyo iliyotokea leo Jumamosi saa tisa na nusu jioni kwenye barabara kuu ya Sotik-Kericho, ilihusisha magari matatu ambayo ni; lori, matatu ya uchukuzi wa abiria na gari ndogo la kibinafsi.

Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali za Kaplong na Kapkatet kwa matibabu.