Watu 13 wafariki kufuatia kulipuka kwa kilipuzi eneo la Elwak

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu 13 wameaga dunia Jumatatu kufuatia mlipuko wa kilipuzi katika eneo la Elwak,kaunti ya Mandera.

Kilipuzi hicho kilikuwa kimefungwa kwenye mzigo uliobebwa na punda.

13 hao waliofariki walijumuisha watu 10 wa kigeni na raia watatu wa kigeni wakiwemo wahudumu wawili wa taxi.

Tukio hilo limetokea karibu na kambi ya maafisa wa utawala

Benki ya Equity imetangaza kusitisha huduma zake katika eneo hilo, kufuatia mlipuko huo ambao mi wa pili katika eneo hilo katikasiku za hivi karibuni.

Waliofariki wanajumuisha Waethiopia watatu,Wakenya watatu na raia wa kigeni saba.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article