Watu 11,000 wametoroka makwao nchini Haiti kwa hofu ya usalama

Dismas Otuke
1 Min Read

Takriban watu 41,000 wamelazimika kuhama makwao nchini Haiti, tangu Novemba 11 mwaka huu kwa ya kiusalama na vita vinavyoendelea.

Makundi ya haki za kibinadamu yanasema idadi kubwa ya waliathiriwa ni watoto wakiwa asilimia 52 ambao ni zaidi ya wataoto 21,000.

Hii ndio idadi kubwa ya watu waliotoroka makwao nchini humo tangu Januari mwaka jana, kwa mjibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM).

Watoto wengi wamelazimika kutafuta hifadhi katika shule zilizosongamana huku wakikosa chakula,maji na huduma za afya.

Pia asilimia 70 ya watoto wamesajiliwa na makundi na magenge nchini Haiti na kudororesha usalama zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Watoto hao wanajiunga na magenge kama njia ya kutafuta riziki huku wengine wakilazimishwa.

Magenge yanathibiti asilimia 85 ya mji mkuu wa Haiti Port-Au Prince, licha ya vikosi vya usalama vya umoja wa mataifa vikiongozi na Kenya kushika doria.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *