Watu wapatao 11 walifariki katika ajali iliyotokea jana jioni katika kijiji cha Kabukome, kata ya Yarubungo, wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera nchini Tanzania.
Watu wengine 16 waliachwa na majeraha kutokana na ajali hiyo iliyohusisha basi la abiria la Kampuni ya Kabiko linalohudumu kati ya Kigoma na Bukoba.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania Innocent Lugha Bashungwa alifika katika eneo la tukio na kuthibitisha ajali hiyo pamoja na idadi ya vifo na majeruhi.
Bashungwa alisema pia kwamba walizuru majeruhi hospitalini akisema kwamba hali yao iko imara huku akishukuru madaktari na wauguzi kwa huduma nzuri.
Waziri huyo alisema kwamba serikali itabadilisha kanuni za Trafiki ili kuhakikisha kwamba madereva wazembe wanachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kunakili vitendo vya na wasipojiboresha wapokonywe leseni kabisa.