Ilikuwa mbwembwe na mahanjam ya kila nui kwa watoto zaidi ya 4,000 mjini Nyahururu, walioandaliwa sherehe ya Krismasi na Askofu wa Dayosisi eneo hilo Meja mstaafu Samson Gachathi mapema leo.
Watoto hao wamepata fursa ya kucheza michezo kadhaa ,na kusherehekea Krismasi iliyoandaliwa na Askofu Gachathi .
Askofu Gachathi aliwahimiza watoto hao kuwa na ujasiri huku akiwapa zawadi kochokocha za kusherehekea Krismasi.
Sherehe za mwaka huu za Krismasi zitaadhimishwa kesho kote duniani ukiwa ukumbusho wa kuzaliwa kwa Masii Yesu Kristo aliyekuwa kuokoa ulimwengu dhidi ya dhambi.