Watoto wawili wafariki kwenye moto mtaani Umoja

Dismas Otuke
1 Min Read

Watoto wawili wa umri wa miaka sita na minane waliangamia katika ajali ya moto Alhamisi usiku katika mtaa wa Umoja Three kaunti ya Nairobi, ambapo nyumba zaidi ya 20 ziliteketea.

Wazima moto waliofika walifanikiwa kuudhibiti moto huo wakisaidiwa na wakazi  walipokumbana na miili ya watoto hao mvulana na msichana.

Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo, huku baadhi ya wakazi wakielezea kuwa ulianzia katika chumba kimoja kabla ya kuenea katika vyumba vingine.

Maiti za watoto hao zilipekekwa katika makafani ya kaunti ya Nairobi kusubiri upasuaji na uchunguzi zaidi.

TAGGED:
Share This Article