Watano waangamia, wengine 18 wajeruhiwa kwa ajali Bomet

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu watano wameripotowa kufariki papo hapo huku wengine 18 wakijeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara ya Olonguruone-Silibwet katika kaunti ya Bomet Jumatatu jioni.

Ajai hiyo ilitokea baada ya gari la abiria la Matatu kugonga  trekta.

Kulingana na mashuhuda, dereva wa matatu hiyo iliyokuwa ikielekea Bomet alikuwa akipita safu ya barabara isiyo yake na alipofika mahali pa ajali, akaigonga trekta.

Majeruhi hao 18 walipelekwa katika hospitai ya kimisheni ya Tenwek ili kutibiwa.

Website |  + posts
Share This Article