Wataalamu wa lishe walalamikia kutengwa kwenye mpango wa afya bora kwa wote

Marion Bosire
1 Min Read

Wataalamu wa lishe humu nchini wamelalamikia kile wanachokitaja kuwa hatua ya kimakusudi ya kuwatenga kwenye mpango wa serikali wa upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote UHC.

Kupitia kwa chama chao, wataalamu hao wa lishe wanapinga kutohusishwa kwao kwenye utekelezaji wa mpango huo wa afya hasa kutumwa kwa wahudumu wa afya wa jamii nyanjani.

Wanachama hao wa chama cha wataalamu wa lishe nchini “Kenya Union of Nutritionists and Dieticians – KUNAD” walizungumza pembezoni mwa kongamano la kisayansi katika bewa la kabete ya juu la chuo kikuu cha Nairobi,.

Mwekahazina wa kitaifa wa chama hicho Lilian Mumina alisema ili mpango huo wa afya ufanikiwe, unahitaji kushirikisha wataalamu wa kada zote za sekta ya afya.

Mumina alielezea kwamba wameandika waraka kwa wizara ya Afya wakitaka wataalamu wa lishe wahusishwe katika utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote UHC.

Share This Article