Wataalam washindwa kubaini chanzo cha kifo kwa baadhi ya miili ya Shakahola

Tom Mathinji
1 Min Read

Wataalam wa upasuaji wa maiti, wanakabiliwa na wakati mgumu kubainisha chanzo cha kifo  kwa baadhi ya maiti iliyofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola, unaohusishwa na mhubiri tata Paul Makenzi.

Kulingana na mpasuaji mkuu wa maiti wa serikali daktari Johansen Oduor, kiwango cha kuharibika kwa miili hiyo, kimesababisha kuto-julikana kwa chanzo cha maafa.

Kulingana na Oduor, uchunguzi wa awali wa miili ulibainisha kuwa chanzo cha maafa kulikuwa ni njaa, huku wengine wakiwa na dalili za kunyongwa au majeraha kutokana na  vifaa butu.

Alisema kundi lake lilifanyia miili 22 uchunguzi, iliyojumuisha miili 13 ya wanawake na miili mitano ya wanaume, huku miili minne ikikosa kubainika ikiwa ni ya kiume au like kutokana na kiwango  cha kuharibika kwa miili hiyo.

Alidokeza kuwa miili hiyo ilijumuisha watoto 14 na watu wazima saba, huku umri wa mwili mmoja ukikosa kubainika.

Kuhusu chanzo cha kifo, Dkt. Oduor alisema watu watatu walikufa kutokana na njaa, lakini kundi lake halikubainisha chanzo cha vifo 19.

Hadi kufikia sasa, kundi lake limefanyia uchunguzi maiti 49, huku zoezi hilo likiwa katika awamu ya tatu lililoanza siku ya Jumanne.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *