Wasimamizi wa vituo vya mtihani wa kitaifa wa KCSE waonywa

Marion Bosire
1 Min Read

Katibu wa elimu ya msingi katika wizara ya elimu Belio Kipsang ameonya wasimamizi wa vituo vya mtihani unaoendelea wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE na walimu wakuu wa shule dhidi ya kukubalia udanganyifu.

Belio anasema kwamba hatua kama hiyo inawaweka katika hatari ya kupoteza ajira.

Kulingana na katibu Kipsang ni visa 11 pekee vilivyoripotiwa vya wasimamizi wa mtihani huo kujaribu kuingiza simu za rununu na vifaa vingine kwenye vituo vya mtihani.

Alisema pia kwamba katika siku za usoni, wizara ya elimu itapunguza idadi ya maafisa wa usalama wanaosimamia vituo vya mtihani kama njia ya kupunguza woga kati ya watahiniwa.

Leo Ijumaa Novemba 8, 2024, watahiniwa wanafanya mtihani wa vitendo wa somo la Kemia. Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE mwaka huu unatarajiwa kukamilika Ijumaa Novemba 22.

Share This Article