Wasimamizi wa shule wahimizwa kudumisha uwajibikaji

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei.

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, amewataka wasimamizi wa shule kote nchini kudumisha uwajibikaji wa hali ya juu wanapotekeleza majukumu yao.

Akizungumza alipoandaa mkutano na wasimamizi wa shule kupitia mtandao, Koskei alisema ipo haja ya kuimarisha nidhamu katika usimamizi wa fedha na rasilimali za umma, akiongeza kuwa mazungumzo hayo yaliangazia kuimarisha viwango vya utaalam katika usimamizi wa taasisi hizo za elimu.

Aidha aliwataka Walimu Wakuu wa shule kushirikiana kwa karibu na Bodi za Usimamizi pamoja na wazazi ili kuboresha viwango vya elimu kwa kila mwanafunzi.

Wakati huo huo, Koskei aliwaonya wasimamizi wa shule dhidi ya kuongeza idadi ya wanafunzi waliosajiliwa ili kuvutia mgao mkubwa zaidi wa serikali akisema hatua hiyo ni ukiukaji wa uwajibikaji.

Aliwahimiza viongozi wa shule na bodi za usimamizi zishughulikia mbinu hafifu za ununuzi wa bidhaa na huduma, mgongano wa maslahi na usimamizi duni wa miradi ya maendeleo shuleni.

TAGGED:
Share This Article