Washukiwa wawili wa wizi wa mifugo wauawa Kakamega

Kbc Digital
1 Min Read

Washukiwa wawili wa wizi wa mifugo walipoteza maisha usiku wa kuamkia jana Jumatatu, baada ya jaribio lao la kuiba mbuzi na nguruwe katika boma moja eneo hilo kugonga mwamba.

Zephania Wamalwa, mmiliki wa mifugo hao, alidai kusikia milio ya mbuzi wake na mara moja akaamka na kugundua kuwa wameibwa. Hii ilimfanya apige mayowe kuomba msaada kutoka kwa majirani zake.

Wakazi wa Eshianini Bulanda wamelalamikia ongezeko la wizi wa mifugo, wakisema kuwa bidhaa zao zimekuwa zikiibwa mara kwa mara.

Aidha, wanakiri kuwaua washukiwa hao wawili baada ya kuwakamata kwenye tukio hilo.

Chifu wa eneo hilo, Shikuku Ham, amethibitisha kuwa washukiwa hao ni wezi sugu waliokuwa wakihangaisha wenyeji.

Hata hivyo, amewataka wakazi kutojichukulia sheria mikononi mwao wanapowakamata.

Taarifa ya Carolyn Necheza 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *