Washukiwa watatu zaidi wakamatwa kuhusiana na mauaji ya Richard Otieno Haga

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa mauaji ya Richard Otieno.

Maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, wamewatia nguvuni washukiwa watatu zaidi, wanaohusishwa na mauaji ya  Richard Otieno Haga, almaarufu Rais wa Molo, yaliyotekelezwa Januari 18,2025 katika eneo la Elburgon, kaunti ya Nakuru.

Washukiwa hao Peter Oketch, almaarufu DJ IO, Joseph Kihara Kariuki, almaarufu Jose, na Evans Aseka Okututi, walihusishwa na mauaji hayo baada ya kutekelezwa kwa uchunguzi wa kimaabara pamoja na washukiwa wengine ambao bado wako mbioni.

Kulingana idara ya DCI kupitia ukurasa wake wa X, washukiwa hao walisafirishwa kutoka Molo hadi Elburgon kutekeleza mauaji hayo.

Mshukiwa wa mauaji ya Richard Otieno.

Baada ya mauaji hayo, Peter Oketch na Joseph Kihara Kariuki walitorokea eneo la Majahida katika wilaya ya  Bariadi nchni Tanzania, kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria. Hata hivyo walirejea hapa nchini Ijumaa Februari 21,2025 baada kuandamwa vikali na maafisa wa Tanzania.

Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani, huku uchunguzi ukiendelea. Maafisa wa DCI wanaendelea kuwatafuta washukiwa zaidi.

Mshukiwa wa mauaji ya Richard Otieno.

Hapo awali maafisa wa DCI waliwakamata washukiwa watano kuhusiana na mauaji ya Richard.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *