Maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI, waliokuwa wakiwasaka majambazi hao, walimtia nguvuni Mutua Julius John mwezi jana, na kupata gari lililokuwa limeibwa lenye nambari za usajili KDR 722K.
Baada ya kuhojiwa na maafisa wa polisi, Mutua alisababisha kukamatwa kwa washukiwa wengine watatu ambao kwa sasa wanazuiliwa katika korokoro za polisi, wakisubiri kufikishwa mahakamani.
Kulingana na DCI, miongoni mwa waliokamatwa ni Simon Mumo Chege, ambaye ana utaalam wa kuhitilafiana na nambari maalum ya chassis ya magari yaliyoibwa.
“Alikamatwa katika eneo Grogon, Jijini Nairobi. Mwingine aliye korokoroni ni Raphael Oloo Kira, anayefahamika kwa utoaji nambari bandia za usajili wa magari pamoja na kubadilisha vioo vya magari,” ilisema DCI Kupitia ukurasa wa X.
Mshukiwa mwingine George Nyakundi Ogoro, anayefahamika kwa kukodisha magari akitumia stakabadhi bandia, pia alitiwa nguvuni.
- Tom Mathinjihttps://swahili.kbc.co.ke/author/tommathinji/
- Tom Mathinjihttps://swahili.kbc.co.ke/author/tommathinji/
- Tom Mathinjihttps://swahili.kbc.co.ke/author/tommathinji/
- Tom Mathinjihttps://swahili.kbc.co.ke/author/tommathinji/