Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati akamatwa na polisi.

Maafisa wa polisi wamewakamata walanguzi wa mihadarati, huku wakiimarisha vita dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya kote nchini.

Katika matukio ya hivi punde, maafisa hao wamewakamata washukiwa wawili katika barabara ya Nambale waliokuwa na bangi ya thamani ya shilingi 1,320,000.

Washukiwa hao Okuchil Ayubu mwenye umri wa miaka 40, na kijana wa umri wa miaka 17, walikuwa wakisafiri ndani ya matatu, ilipoamriwa kusimama katika kizuizi cha polisi.

Baada ya mizigo yao kupekuliwa, maafisa hao wa polisi walipata kilo 44 za bangi.

Wakati huo huo, maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria katika eneo la Biamati kwenye barabara ya Mutemorabu – Boembu waliwanasa washukiwa waliokuwa wakijiandaa kusafirisha kilo 260 za bangi za thamani ya shilingi 7,800,000.

Washukiwa hao wanazuiliwa, wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Kupitia mtandao wa X, idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI, iliwashukuru wananchi kwa kuendelea kutoa habari, huku ikihakikishia umma kujitolea kwake kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya.

TAGGED:
Share This Article