Washukiwa 4 wa biashara haramu ya dhahabu wakamatwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka kitengo cha Operation Support Unit (OSU), wamewakamata  washukiwa wanne wanaodaiwa kuendesha biashara haramu ya dhahabu.

Washukiwa hao Patroba Odhiambo Tobias, Isaac Forkay Sleyon, Omong Ekoume Louis na Wadja Bangsi Tang, walitiwa mbaroni wakati wa operesheni kwenye nyumba moja ya makazi mtaa wa Gigiri,barabara ya  Whispers Avenue.

Makachero hao walinasa mashini ya kuyeyusha dhahabu pamoja na vifaa vingine ikiwemo mihuri ya kampuni za Alaska Express Freight Group Ltd, Longcrane Logistics Limited na Kakan Traders and Company pamoja na stakabadhi kadha.

“Uchunguzi umebaini kwamba kampuni  ya Alaska Express Freight Group na  pia imehusishwa kwenye malalamishi yaliowasilishwa na raia wawili wa Canada waliolaghaiwa dola 27,500 wiki jana,” ilisema idara ya DCI kupitia ukurasa wake wa X

Washukiwa hao kwa sasa wanahojiwa na maafisa hao wa polisi kabla ya kufikishwa mahakamani.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article