Shirikisho la Riadha Ulimwenguni limetangaza zawadi ya pesa ya shilingi milioni 6.5 kwa kila mshindi wa nishani ya dhahabu ya Olimpiki kaunzia kwa makalaya mwaka huu jijini Paris Ufaransa.
Itakuwa mara ya kwanza kwa zawadi ya pesa kutolewa katika michezo ya Olimpiki .
Kwa jumla shirikisho la riadha Ulimwenguni limetenga shilingi milioni 312 kuwatuza washindi wa dhahabu katika fainali zote 48 za riadha, ikiwemo mbio za kupokezana kijiti ambao pia watapokea kiasi sawa cha shilingi milioni 6 .5.