Washindi wa dhahabu na shaba wapandishwa vyeo kwa polisi

Marion Bosire
1 Min Read

Beatrice Chebet na Abraham Kibiwot, wamepandishwa ngazi leo Jumatano hadi vyeo vya koplo baada ya ushindi wa medali za dhahabu na shaba mtawalia katika mashindano ya Olimpiki yaliyokamilika hivi maajuzi mjini ParisUfaransa.

Chebet ambaye alikuwa bingwa mtetezi wa mbio za mita 10,000, alishinda mbio hizo tena na kunyakua pia za mita 5000 huku Kibiwot akipata shaba kwa mita 3000.

Hafla hiyo iliyofanyika katika jumba la Jogoo mjini Nairobi ikiongozwa na kaimu afisa mkuu wa polisi Gilbert Masengeli, pia ilihudhuriwa na naibu anayesimamia askari wa kawaida Eliud Lagat, mshindi wa dhahabu na shaba wa mita 800 – Emmanuel Wanyonyi na koplo Mary Moraa mtawalia na mrusha mkuki sajenti mkuu Julius Yego.

Masengeli aliwapongeza kwa ushindi na kutaja nidhamu na bidii kuwa iliyopelekea kunawiri huku akiwataka kujiepusha na ulaji mku.

Naye Lagat pia aliwapongeza na kuongeza kuwa ushindi huo ni dhibitisho ya jinsi idara ya polisi inavyotilia mkazo maswala ya michezo kwenye idara hiyo.

Katika Mashindano hayo ya takribani wiki tatu, Kenya iliebuka ya kwanza Afrika na namabari 17 duniani kwa ujumla wa medali 11- nne za dhahabu, mbili za fedha na tano za shaba. Kati yazo, kikosi hicho cha usalama wa ndani kinajivunia medali nne.

Share This Article