Wasafi kutambulisha msanii mgeni kesho

Marion Bosire
1 Min Read

Kampuni ya kusimamia wanamuziki Tanzania kwa jina Wasafi Classic Baby – WCB inapanga kutamblisha msanii mgeni kesho Novemba 16, 2023.

Wahusika wa kampuni hiyo akiwemo mmiliki wake Diamond Platnumz wameonekana kwenye video wakitaja sifa za msanii huyo.

Wanasema kwamba ana talanta ya kupigiwa mfano, ana sura nzuri, anachangamsha sana akiwa jukwaani, anajua sana kuandika nyimbo na kwamba amekomaa kiakili.

Haya yanajiri miaka mitatu tangu kampuni hiyo ilipozindua rasmi msanii wa kike Zuchu.

Wasanii waliosajiliwa kwenye kampuni hiyo ni Diamond Platnumz, Rayvanny, Lava Lava, Mbosso, Queen Darleen na Zuchu.

Share This Article