Waraibu wa vileo vya mvinyo na pombe katika kaunti ya Kirinyaga wamepatwa na pigo baada ya Gavana wa kaunti ya hiyo Anne Waiguru kutoa agizo la kufungwa kwa baaa zote na maeneo ya kuuza pombe mapema Jumamosi.
Waiguru ameelezea kutamaushwa kwake na ufisadi uliokithiri katika utoaji wa leseni za wamiliki wa baa na maeneo ya kuuza pombe na kuanzisha uchunguzi wa kubaini uhalali wa leseni zilizotolewa.
Gavana huyo alitoa amri hiyo alipohudhuria mazishi ya watu 17 waliofariki baada ya kubugia pombe haramu.