Wapiga muziki Nigeria wapiga marufuku muziki wa Burnaboy

Burna Boy alinakiliwa kwenye video akimshambulia DJ Tunez katika hafla fulani jijini Lagos.

Marion Bosire
1 Min Read

Muungano wa wapiga muziki nchini Nigeria umetangaza marufuku ya muda kwa nyimbo zote za mwanamuziki Burna Boy na kuelekeza wapiga muziki wote nchini Nigeria na ughaibuni kuondoa nyimbo hizo.

Hatua hii inafuatia kisa kilichonakiliwa kwenye video iliyosambaa mtandaoni ambapo Burna anaonekana akimpiga DJ Tunez katika hafla moja ya nyumbani jijini Lagos.

Katika taarifa, muungano huo wa wapiga muziki ulidhihirisha umoja na DJ Tunez na kuelekeza wapiga muziki wote wasimame naye huku wakidumisha utaalamu katika tasnia ya burudani.

Chama hicho kilieleza kuwa hakuna mtu anayezaliwa akimchukia mtu mwingine kwa sababu ya rangi ya ngozi, dini, asili au jinsia yake.

“Wapendwa NDJ, hakuna mtu anayezaliwa akimchukia mwingine kwa sababu ya rangi ya ngozi, dini, asili au jinsia. Watu hujifunza kuchukia, na ikiwa wanaweza kujifunza kuchukia, basi wanaweza pia kufundishwa kupenda kwa kuwa upendo huja kiasili zaidi katika moyo wa mwanadamu kuliko kinyume chake.” ilisema taarifa hiyo.

Wapiga muziki walihimizwa kuwa wavumilivu kukataa chuki au ubaguzi unaotokana na tabaka, imani, dhehebu, dini au jinsia huku wakihakikisha uhuru na usawa ili waweze kustawi.

Share This Article