Wapatanishi wa Israel waagizwa kutoka Qatar

Tom Mathinji, BBC and BBC
1 Min Read
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Maafisa wa kijasusi wa Israel wameagizwa kuondoka Qatar baada ya mazungumzo ya kusitisha mapigano “kukwama”, shirika la kijasusi la Mossad limesema.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel, Mossad inasema mkuu wake David Barnea “aliamuru timu yake huko Doha kurejea Israel” baada ya kuagizwa kufanya hivyo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

“Shirika la kigaidi la Hamas halikutimiza sehemu yake ya makubaliano, ambayo ni pamoja na kuachiliwa kwa watoto na wanawake wote kulingana na orodha ambayo ilitolewa kwa Hamas na kuidhinishwa nayo,” inaongeza.

Qatar imekuwa mpatanishi katika mazungumzo kati ya Hamas na Israel tangu vita vilipozuka, ikiwa na jukumu muhimu katika kuandaa na kuongeza muda wa usitishaji mapigano kwa wiki moja na kutolewa kwa mateka.

Website |  + posts
Share This Article