Wapalestina 67 waangamizwa na majeshi ya Israel wakisubiri msaada wa chakula

Dismas Otuke
1 Min Read

Wapalestina 67 wameripotiwa kuuawa  na wanajeshi wa Israel wakisubiri chakula cha msaada kutoka kwa  malori ya Umoja wa Mataifa, UN katika Ukanda wa Gaza mapema Jumapili.

Mashambulizi hayo yalijiri huku  Israel ikitoa tahadhari kwa wakazi wa Gaza kuondoka eneo hilo.

Malori 25 yaliyokuwa na misaada ya UN yaliwasili Ukanda wa Gaza ambapo kulikuwa na foleni ndefu za raia wali0subiri misaada hiyo.

Punde si punde, wanajeshi wa Israel walimimina risasi na kuwaua takriban 88 kati yao huku makumi ya wengine wakijeruhiwa siku ya Jumapili.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article