Maelfu ya waombolezaji wamemiminika mapema Jumamosi kumpa buriani mpiganiaji wa uhuru nchini Afrika Kusini mwanawe mfalme wa Zulu, Mangosuthu Buthelezi,aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Marehemu Buthelezi alikuwa mwanzilishi wa chama maarufu cha upaganiaji uhuru wa Afrika Kusini Inkatha Freedom Party (IFP), na aliaga dunia wiki jana..
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,anatarajiwa kutoa hotuba ya rambi rambi kwenye mazishi hayo.
Umaarufu wa chama cha IFP ulidorora wakati kulizuka vita kati ya wafuasi wa chama hicho na kile tawala cha ANC na kusababisha vifo vya watu 12,000 mwaka 1994 ndiposa hayati Rais Nelson Mandela akamteua Buthelezi kuwa waziri wa masuala ya ndani.