Mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mbio za mita 800 Emmanuel Wanyonyi atawinda ushindi wa kwanza wa Diamond League, atakaposhiriki mkondo wa tatu Jumapili hii mjini Rabat Morocco.
Wanyonyi ambaye pia alihifadhi taji ya Kip Keino Classic mwezi Jana atakabiliana na Wycliff Kinyamal, aliyemaliza wa pili katika mikondo miwili ya kwanza pamoja na bingwa wa Olimpiki Emmanuel Korir.
Mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji wanaume zitamshirikisha mshindi wa nishani ya fedha ya dunia Abraham Kibiwott, atakayepimana nguvu na Mkenya mwenza Benjamin Kigen, bingwa wa Olimpiki Soufiane El Bakkali wa Morocco na Samuel Firehu wa Ethiopia.