Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi amewaongoza wakazi wa mtaa wa Githogoro katika wadi ya Karura kuandamana kupinga unyakuzi wa ardhi ya umma.
Shamba hilo linalozozaniwa ni na ekari 15 katika eneo la Githogoro karibu na barabara ya Kiambu na yamkini limetwaliwa na mstawishaji wa kibinafsi ambaye alikuwa ameweka ua.
Wakazi hao waliojawa na hamaki waliporomosha ua huo.
Akiwahutubia wananchi Wanyonyi amelaani kitendo hicho cha unyakuzi wa ardhi ya umma na watu binafsi.
Aliahidi kushirikiana na tume ya ardhi nchini, ili kuwaleta masoroveya kupima shamba hilo la umma.
Kulingana na mzee wa kijiji hicho kwa jina Wamalwa ,wanyakuzi wa shamba hilo wamejaribu kuligawanyisha kwa vipande vidogo kinyume cha sehria.