Wanyonyi atangaza kuwania uenyekiti wa ODM Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi amejitosa kwenye kinyang’anyirio cha Uenyekiti wa chama cha Orange Democratic movement(ODM) katika kaunti ya Nairobi.

Akizungumza jana katika kanisa la   Africa Inland Church wadi  ya Sarangombe eneo bunge la  Kibra ,Wanyonyi alisema lengo lake la kuwania wadhfa huo ni kubadilisha uongozi wa chama na kuleta ari mpya kukiandaa chama cha ODM kwa chaguzi zijazo.

“Ninataka mnipe fursa niwe mwenyekiti wa ODM kaunti ya Nairobi,tunataka nguvu mpya katika chama chetu ,fikra mpya  na tujiandae kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.”akasema Wanyonyi

Wanyonyi amefichua pia lengo lake la kuwania Ugavana wa kaunti ya Nairobi kwenye uchaguzi wa mwaka 2027 .
Aidha Wanyonyi alisisitiza haja ODM kuandaa uchaguzi huru na wa haki, ili kumaliza mizozo na malumbano ambayo yamekuwa yakishuhudiwa chamani.
Chama cha Odm kinatarajiwa kuandaa uchaguzi wake wiki hii baada ya zoezi hilo kuahirishwa mara kadhaa.
Website |  + posts
Share This Article