Wanjiru kuteta taji ya Berlin Marathon Jumapili hii

Mbio za wanaume zinatarajia kupata bingwa mpya kufuatia kujiondoa kwa mshikilizi wa rekodi ya dunia Sabastian Sawe aliyetwaa ushindi mwaka jana .

Dismas Otuke
1 Min Read

Rosemary Wanjiru wa Kenya atarejea kwenye barabara za Berlin nchini Ujerumani Jumapili hii Septemba 27, kutetea taji yake ya mwaka jana ya Berlin Marathon.

Wanjiru ambaye ni wa pili katika kasi kati ya washiriki wa mwaka huu atakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia Tigst Assefa

,Bedatu Hirpa na Dera Dida wote kutoka Ethiopia.

Mbio za wanaume zinatarajia kupata bingwa mpya kufuatia kujiondoa kwa mshikilizi wa rekodi ya dunia Sabastian Sawe aliyetwaa ushindi mwaka jana .

Aidha,mwanariadha mkongwe Kenenisa Bekele wa Ethiopia ambaye ndiye mwenye kasi zaidi kati ya washiriki wa mwaka huu alilazimika pia kujiondoa.

Waethiopia wametawala orodha ya washiriki katika mbio za wanaume wakiwemo Selemon Barega,Gataneh Mola,Guye Adola wakipambana na bingwa wa dunia Gabriel Geay wa Tanzania pamoja na Mkenya pekee Eric Sang.

Share This Article