Wanja kupumzishwa Ijumaa hii

Dismas Otuke
1 Min Read

Setter mstaafu wa timu taifa ya Voliboli kwa wanawake marehemu Janet Wanja atazikwa Ijumaa hii Januari 3 katika makaburi ya Lang’ata.

Taarifa kutoka kwa familia imefafanua kuwa kutakuwa na mikutano ya kuandaa mazishi leo , kesho na kesho kutwa katika Hoteli ya Sports View Kasarani,kabla ya ibada ya kuwasha mishumaa kufanyika nyumbani kwake Kasarani kesho kuanzia saa moja usiku.

Misa ya wafu kwa umma itaandaliwa Januari 2 katika ukumbi wa uwanja wa kimataifa wa Kasarani kati ya saa nne asubuhi na saa nane adhuhuri .

Mazishi ya mwendazake yataandaliwa Ijumaa Januari 3 katika makaburi ya Lang’ata.

Wanja alifariki  wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 40 kutokana na saratani.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *