Wanariadha wapata bima ya uzeeni

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Riadha Kenya kimeshirikiana na kampuni ya CPF kutoa bima ya malipo ya uzeeni kwa wanariadha waliostfaafu na wale wangali uwanjani.

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amewataka wanariadha wote nchini kusijalili kupitia kwa chama cha riadha ili kunufaika na bima hiyo.

Wanariadha ambao wangali mashindanoni watalazimika kuchangia bima hiyo ili kunufaika.

Wizara ya michezo ilitoa mchango wa shilingi milioni kwa hazina hiyo .

Rais wa Chama cha Riadha Kenya alisisitiza umuhimu wa wanariadha kukumbatia bima hiyo ili kutotaabika baada ya kustaafu.

Share This Article