Wanariadha wa kenya watakaoshiriki michezo ya Olimpiki wanatarajiwa kuripoti kwa kambi ya mazoezi Jumapili hii Juni 23 chini ya mpangilio mpya wa mazoezi.
Kulingana na mpangilio huo mpyawanariadha wa mbio za masafa mafupi za mita 100,mita 400,mita 400 kuruka viunzi na mita 800 watakita kambi ya mazoezi Uwanjani Kasarani.
Naibu kiongozi wa ujumbe wa Kenya wa Olimpiki Barnaba Korir, amefafanua kuwa wanariadha wa mbio za mita 1500,mita 3000 kuruka viunzi na maji,mita 5,000 na mita 10,000 watakita kambi ya mazoezi katika kambi ya Kazi mingi iliyo mjini Eldoret.
Wanariadha watapewa makocha maalum wakati wa mazoezi ili kuhakisha wako shwari kwa Olimpiki ambapo fani ya riadha itaandaliwa kati ya Agosti 1 na 11 .
Kadhalika wanariadha wa mbio za mita 100,400 na 400 kuruka viunzi watapiga kambi ya mazoezi kuanzia Julai 8 hadi 30.
Waanariadha wa mbio za marathon tayari wako kambini mjini Iten kujiandaa kwa mashindano hayo.
Kulingana na Korir wanaradha zaidi wanatarajiwa kutimiza muda wa kufuzu kufikia Juni 30 ambayo ndiyo siku ya mwisho kufuzu.
Wanariadha wanaowania muda wa kufuzu ni pamoja na Sarah Moraa na Julius Yego.