Wanariadha wapatao 50 wa kigeni wamealikwa kushiriki makala ya 3 ya mbio za nyika za Sirikwa Classic, zitakazoandaliwa eneo la Lobo Village mjini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu Februari 3 mwaka huu.
Kulingana na Mkurugenzi wa mashindano hayo Barnaba Korir, wanariadha walioalikwa ni wa kutoka mataifa ya Uganda,Ethiopia,Tanzania na Eritrea huku orodha ya mwisho ikibainika mwishoni mwa mwezi huu.
Korir pia amedokeza kuwa huenda chama cha Riadha Kenya kikatumia mashindano hayo kuteua timu itakayoshiriki mashindano ya dunia ya mbio za nyika Machi 30 mjini Belgrade Serbia.
Vitengo vitakavyoshindaniwa katika makala ya waka huu ni kilomita 10 kwa wanaume na wanawake,kilomita 6 wasichana ,kilomita 8 wavulana,mbio za watoto na mbio za wakongwe walio zaidi ya umri wa miaka 45.