Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga, ametoa onyo kali kwa watu wanaojihusiaha na ghasia na uharibifu wa Mali wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.
Kupitia kwa taarifa, Ingonga aliagiza idara ya upelelezi wa makosa ya jinai(DCI), kukamilisha uchunguzi kuhusiana na ghasia na uharibifu wa Mali na kuwasilisha matokeo kwa mwongozo zaidi.
Mkurugenzi huyo ameonya dhidi ya ghasia na uharibifu zaidi wa Mali , alidokeza kuwa wanaoshiriki maandamano wanapaswa kudumisha amani, na hawapaswi kuwa na silaha.
Igonga aliongeza kuwa katiba ya Kenya ya mwaka 2010, inalinda haki ya kila mkenya kishirikii maandamano na kuwasilisha malalamushi katika aafisi za umma.
Alisema visa vyovyote vya ghasia vitakavyosababiaha kupotea kwa maisha, uharibifu wa Mali ya umma na kibinafsi, vitakabiliwa kikamilifu na sheria.
Matamshi ya Ingonga yanajiri baada ya Mali kuharibiwa ikiwa ni pamoja na majengo y bunge wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.