Wanakijiji wateketeza nyumba nne Siaya kufuatia mauaji ya watu tisa

Haya ni baada ya kukamatwa kwa mke wa mshukiwa mkuu wa mauaji hayo ambaye pia alipatikana na chupa kadhaa zilizojaa mafuta ya petroli chumbani mwake.

Boniface Musotsi
1 Min Read

Wakaazi wenye hamaki katika kijiji cha upanda – Ugunja kaunti ya Siaya, wamelipiza kisasi kwa kuteketeza nyumba nne na kuharibu mali mbalimbali za mshukiwa mkuu wa mauaji ya watu tisa.

Haya ni baada ya kukamatwa kwa mke wa mshukiwa mkuu wa mauaji hayo ambaye pia alipatikana na chupa kadhaa zilizojaa mafuta ya petroli chumbani mwake.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika, watu wasiojulikana walivamia nyuma ya tisa hao wakati wa usiku na kufunga mlango kwa nje kisha wakawasha moto kwenye nyumba hiyo kwa kutumia petroli na kusababisha vifo vya baba, mama na wanao saba wenye kati ya umri wa miaka 17 na miezi sita.

Miili ya tisa hao imehifadhiwa katika makavazi ya hospitali ya Ambira ikingoja kufanyiwa upasuaji.
Aliyekamatwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Ugunja wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.

Boniface Musotsi
+ posts
Share This Article