Jeshi la Ulinzi (IDF), la Israel limesema kuwa wanajeshi wake wanne wameuawa kusini mwa Lebanon, ambako majeshi yake yanakabiliana na wapiganaji wa Hezbollah.
Jeshi la Israel lilianzisha mashambulizi ya nchi kavu nchini Lebanon, katika juhudi za kuangamiza kundi la Hezbollah.
Kupitia kwa taarifa siku ya Jumanne, IDF iliwataja wanajeshi watatu waliofariki kwenye mapigano ambao ni Kapteni Noam Madmoni mwenye umri wa miaka 22, sajenti Ben Cohen, 21, na sajenti Maxsim Entis 22.
Katika taarifa tofauti, IDF ilisema mwanajeshi mwingine aliuawa huku wengine wawili wakijeruhiwa kwenye vita hivyo.
Maafisa hao wawili walipelekwa hospitalini huyu mwanajeshi mmoja akitajwa kuwa mahututi.
Israel ilianzisha mashambulizi ya nchi kavu nchini Lebanon, baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu kuagiza wanajeshi kupanua mashambulizi yao kusini mwa Lebanon.