Wanajeshi wanane wa Peru wameaga dunia, rubani mmoja akinusurika akiwa na majeraha mabaya baada ya helikopta ya Jeshi la Anga la Peru aina ya Mi-17 kuanguka kusini-mashariki mwa nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Peru ilitangaza ajali hiyo siku ya Ijumaa, baada ya ndege hiyo kuripotiwa kupotea Alhamisi usiku katika mkoa wa Ayacucho, bonde la mito ya Apurímac.
Helikopta hiyo ilikuwa katika shughuli ya kuwaokoa wanajeshi watatu, ambao ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
Kati ya wanajeshi tisa waliokuwemo kwenye helikopta hiyo, watano walikuwa wa jeshi la anga na watatu wa Jeshi la nchi kavu, huku rubani aliyenusurika, kamanda Enzo Espinoza Roque, akisafirishwa hadi Lima kwa matibabu maalumu.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na mamlaka zinaendelea na uchunguzi.