Hali inazidi kuwa tete nchini Madagascar baada ya wanajeshi kujiunga na waandamanaji vijana wa Gen Z, wanaotaka kujiuzulu kwa Rais Andriy Rajoelina.
Wanajeshi walijiunga na vijana wa Gen Z Jumamosi katikati ya mji mkuu wa Antananarivo kupinga huduma mbovu za serikali.
Wengi wa wanajeshi hao ni wale waliomuunga mkono Rais Rajoelina kutwaa mamlaka kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16 kufuatia maandamano ya kitaifa.
Katika hatua ya kukaidi, Rais Rajoelina alipuuza jaribio hilo la kupindua serikali na kuwataka wanajeshi kulinda katiba.
Rais wanaandamana nchini Madagascar kupinga kukatizwa kwa maji na umeme mara kwa mara chini ya utawala wa Rajoelina.