Wanajeshi wa Kenya waua wanamgambo 6 wa Al Shabaab Lamu

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanajeshi wa Kenya waliwauwa wanamgambo sita wa kundi haramu la Al Shabaab, katika msako ulioendesha kaunti ya Lamu Jumatano wiki hii.

Kulingana na taarifa hiyo waliouawa ni pamoja na mpiganaji wa kigeni .

Wanajeshi wa Kenya walitekeleza shambulizi hilo katika msako uliotekelezwa saa saba adhuhuri karibu na maficho ya Al Shabaa eneo la Kumba, yapata kilomita 10 kutoka Pandanguo viungani mwa msitu wa Boni.

Maafisa wa KDF walisema baadhi ya wanamgambo walifanikiwa kutoroka na majeraha, huku silaha kadhaa zikipatikana.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article