Wanajeshi kadhaa wanahofiwa kufariki jana Jumapili usiku, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga vilipuzi katika msitu wa Boni kaunti ya Lamu, kwenye shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na kundi la Al-Shabaab.
Yamkini idadi isiyojulikana ya wanajeshi wameuawa na kujeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo.
Msemaji wa wanajeshi Brigadia Ziporah Kioko mapema leo Jumatatu amethibitisha kuwa gari hilo lilipuliwa kwa bomu lililokuwa limetegwa barabarani na Al-Shabaab, wanajeshi wakiwa katika zamu ya kushika doria katika barabara ya Bodhei-Majengo.
Wanajeshi wamewaomba raia kutoa taarifa kuhusiana na visa vyovyote wanavyoshuku kuwa vya Al-Shabaab.