Wanahabari wahimizwa kupiga jeki vita dhidi ya ufisadi

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwenyekiti wa EACC Abdi Mohamud.

Wanahabari wamehimizwa kupiga jeki vita dhidi ya ufisadi kwa kufichua visa vya ufisadi na hali ya kutojali sheria kupitia vyombo vya habari.

Mwenyekiti wa Tume ya Maadili na vita dhidi ya Ufisadi (EACC), Abdi Ahmed alisema vita dhdi ya uovu huo vinapaswa kuimarishwa, huku ufisadi ukiendelea kuongezeka hapa nchini.

Akizungumza leo Jumanne, kwenye warsha ya kupambana na ufisadi iliyoandaliwa kwa wanahabari jijini Nairobi, Ahmed alihimiza wanahabari kufanya uchunguzi wa kina zaidi ili kusaidia kufichua visa vya ufisadi hapa nchini.

Mwenyekiti wa tume hiyo David Oginde, alisema wanahabari hutekeleza jukumu muhimu, akidokeza kuwa wao ndio macho yanayoona gizani.

“Wanahabari hutekeleza jukumu muhimu. Ufisadi huharibu mataifa, hutekelezwa kwa siri….wanahabari ni macho yanayoona gizani. Tunapaswa kushirikiana pamoja,” alisema Oginde.

Aidha aliisitiza kuwa tume hiyo imejizatiti kuimarisha mifumo ya kuzuia ufisadi, pamoja na kuongeza uwajibikaji na utekelezaji wa sheria katika taasisi za umma.

Jaji wa Mahakama ya Rufaa Patrick Kiage alisema vyombo vya habari vinapaswa kufichua ufisadi na utovu wa maadili katika jamii.

“Vita dhidi ya ufisadi ni jukumu la kitaifa la kila mmoja,” alisema Jaji Kiage.

Share This Article